Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Sanga Mwalugesha, Wilaya ya Maswa?

Supplementary Question 1

MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri sana ya Serikali, lakini nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Kata ya Binza ni kata ambayo ni kubwa sana, ina wakazi zaidi ya 21,000 lakini haina kituo cha afya. Wananchi wale wamejitahidi, wana eneo kubwa sana ambalo ni zaidi ya hekari 15, lakini Serikali haijajenga. Je, ni lini watajenga kituo cha afya kwenye hiyo Kata ya Binza?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer


NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Minza Mjika kwa swali lake zuri sana. Serikali katika kipindi cha miaka minne ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji wa jumla shilingi bilioni 916 katika kuimarisha huduma za afya msingi, kwa maana ya kwenda kuendeleza miundombinu, kununua vifaa na vifaa tiba lakini pia kutengeneza rasilimali watu kwa ajili ya kutoa huduma hizi za afya.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali mpaka wakati huu imeshajenga jumla ya vituo vya afya 601 katika kipindi cha miaka minne tu.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itaendelea kufikia maeneo yote yale ambayo ni ya kimkakati na yana vigezo, kata zote ambazo zina vigezo vinavyohitajika kujenga vituo vya afya vitafikiwa kwa awamu ili kuhakikisha kwamba miundombinu na huduma hizi za afya msingi zinaweza kuwafikia wananchi na zinaweza kuwasaidia kupata huduma bora ya afya.

Name

Anton Albert Mwantona

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rungwe

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Sanga Mwalugesha, Wilaya ya Maswa?

Supplementary Question 2

MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha kimkakati katika Kata ya Mkunga? Ahsante.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa sababu Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa huduma hii ya afya msingi, na kwa sababu 75% ya jumla ya Watanzania wote wanatengemea kupata huduma ya afya katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya msingi ikiwemo vituo vya afya, nimhakikishie kuwa Serikali inaendelea na mikakati ya kuleta fedha kufikia maeneo mbalimbali kwa ajili ya kujenga vituo vya Afya.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, katika jimbo lake katika mwaka huu wa fedha zitaletwa jumla ya shilingi milioni 250 za kuanza kujenga miundombinu ya awali ya kituo cha afya cha kimkakati katika eneo ambalo wataliteua. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama kata hii aliyoitaja ndiyo eneo la kimakakati katika jimbo lake, Serikali inaleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya. (Makofi)

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Sanga Mwalugesha, Wilaya ya Maswa?

Supplementary Question 3

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi, mwaka 2024 Wizara ya TAMISEMI ilituletea fomu hapa Wabunge wote tukajaza vituo vyetu vya kimkakati kwenye majimbo na mpaka sasa hivi kwenye maeneo hayo wananchi wakafanya sherehe kubwa sana kulingana na changamoto za kiafya ambazo wanapata kwenye maeneo hayo. Je, Wizara ya TAMISEMI hawaoni kuwa kuna umuhimu wa kutupa tarehe maalum, kwamba ni lini vituo hivyo vitajengwa kwenye jimbo langu Kituo cha Kata cha Ivuna na Wabunge wenzangu waliokuwa wametaja kwenye maeneo yao? Ahsante.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali zuri kabisa hili la Mheshimiwa Condester Sichalwe. Kwanza naomba nimhakikishie kwamba Serikali ina nia thabiti ya kujenga vituo hivi vya afya vya kimkakati katika kila jimbo; na ndiyo maana katika mwaka huu wa fedha zitaletwa jumla ya shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuanza kujenga miundombinu ya msingi katika vituo vya afya ambako Waheshimiwa Wabunge mliainisha maeneo ya kimkakati ya kujenga. Kwa hiyo, niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge wote pamoja na Mheshimiwa Mbunge Condester Sichalwe kwamba wananchi wetu tuendelee kuwaambia washerehekee. Mkakati wa Serikali wa kuleta fedha hizi kwa ajili ya kujenga vituo vya afya hivi vya kimkakati kila jimbo upo palepale. Lini? Ni mwaka huu wa bajeti.

Name

Sylivia Francis Sigula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Sanga Mwalugesha, Wilaya ya Maswa?

Supplementary Question 4

MHE. SYLVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Wilaya ya Nkasi, Kata ya Sintali hakuna Kituo cha Afya, hivyo wananchi wanalazimika kufuata huduma mbali. Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Sintali?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Sylivia Sigula kwa swali lake zuri kabisa kwa maslahi ya wananchi, hasa ukizingatia kwamba huduma za afya msingi ni huduma zinazotarajiwa na Watanzania wengi.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ina nia na madhumuni ya kuyafikia maeneo mengi zaidi kwa kupeleka fedha kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya kutolea huduma za afya msingi. Tayari Waheshimiwa Wabunge wote walishajaza fomu za kuainisha maeneo ya kimkakati katika majimbo yao kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivi vya afya.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika jimbo na eneo hili alilolitaja, kama ni miongoni mwa maeneo ya kimkakati, basi fedha zinakuja, shilingi milioni 250, kwa ajili ya kuanza kujenga kituo cha afya hicho cha kimkakati.

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Sanga Mwalugesha, Wilaya ya Maswa?

Supplementary Question 5

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa majimbo yetu yana ukubwa tofauti, kwa mfano Jimbo la Hanang tuna kata 33 na mahitaji ni makubwa, je, Serikali ipo tayari kupeleka fedha kwenye Kata ya Hidet na Balangdalalu ili vituo vya afya viweze kujengwa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Hhayuma kwamba Serikali kwa kutambua umuhimu mkubwa sana wa huduma za afya msingi, inafanya uwekezaji mkubwa wa kuhakikisha inaimarisha huduma hizi za afya msingi katika maeneo yote. Hata kwenye jimbo lake la Hanang Serikali inakusudia kuendelea kufanya uwekezaji kwa kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za afya msingi ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Serikali itaendelea kufanya hivyo kupitia Serikali Kuu pamoja na mapato ya ndani ya halmashauri kujenga vituo vya afya, kuimarisha kujenga zahanati na kuimarisha huduma za afya msingi kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Spika, tayari katika majibu ya awali niliainisha kwamba Serikali katika mwaka huu wa fedha italeta jumla ya shilingi milioni 250 katika kila jimbo kwa ajili ya kuanza kujenga miundombinu ya vituo vya afya. Nimhakikishie kwamba fedha hizo zitakuja.

Mheshimiwa Spika, bado tunaendelea kuzihimiza Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa kupitia mapato ya ndani kutenga fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu hii muhimu katika sekta ya afya pia, ahsante.

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Sanga Mwalugesha, Wilaya ya Maswa?

Supplementary Question 6

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itakamilisha maboma ambayo yamejengwa na wananchi katika Jimbo la Busokelo, hususan Kata ya Kambasegela, Kisegese, Lupigi na Mpombo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Atupele Mwakibete kwamba Serikali inatambua kuwa wananchi baada ya kuhamasika walichangia kwenye maendeleo ya nchi kwa kuanza kujenga maboma katika sekta ya afya.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa Serikali ina dhamira ya dhati kabisa ya kuunga mkono jitihada hizi ambazo zimeanza kuonyeshwa na wananchi, kwa wao wenyewe kuanza kujitolea, na Serikali itaziunga mkono. Tayari kuna fedha ambazo huwa zinaletwa na zinatengwa kupitia bajeti ya Serikali Kuu.

Mheshimiwa Spika, vilevile kupitia Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa, kupitia mapato ya ndani ya halmashauri, Serikali itaendelea kutenga fedha na kuzileta kwa ajili ya kuunga mkono jitihada nzuri kabisa za wananchi za ujenzi na kuendeleza miundombinu katika sekta ya afya. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hata katika jimbo lake jitihada hizo zitaendelea kufanyika.

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri sana ya Serikali aliyoyatoa. Nimeona nisimame ili nimfungulie, maana ameshahojiwa maswali mengi sana. Yale yote aliyoyajibu tumeongea na Wizara ya TAMISEMI. Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ya CCM, tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya vituo vyote hivyo ambavyo Mheshimiwa Naibu Waziri amevisema.

Mheshimiwa Spika, fedha hiyo inaenda sambamba pamoja na maboma ambayo wananchi wamechagia kuyajenga kwa upande wa elimu pamoja na afya. Tuko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha kutoa fedha. Kwa hiyo, ndani ya mwaka huu wa fedha, kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, tutaanza utekelezaji na ukamilishwaji wa maboma ambayo yalishajengwa, nashukuru.