Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 4 | Enviroment | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 56 | 2025-01-31 |
Name
Naghenjwa Livingstone Kaboyoka
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa tope lililojaa katika Bwawa la Kalemawe – Same?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imechukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha inaondoa tope lililojaa katika Bwawa la Kalemawe – Same ikiwa ni pamoja na kukamilisha kazi ya usanifu wa kina na kuandaa gharama kwa ajili ya ukarabati wa bwawa hilo kwa kuondoa tope, kukarabati utoro wa maji, kujenga msingi wa tuta na tuta la bwawa.
Mheshimiwa Spika, pia, Serikali kupitia Wizara ya Maji imetenga fedha, shilingi bilioni moja, ambapo ukarabati umepangwa kufanyika katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2024/2025, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved