Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Naghenjwa Livingstone Kaboyoka
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa tope lililojaa katika Bwawa la Kalemawe – Same?
Supplementary Question 1
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa kazi hii ya kutoa tope katika Bwawa hili la Kalemawe imechukua miaka mingi sana na hivyo kuathiri kazi za kiuchumi za Wilaya ya Same hasa Jimbo la Same Mashariki kwa upande wa uvuvi na umwagiliaji, je, Waziri anaweza kuniambia kwamba anakadiria kazi hii itachukua muda gani? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwa kuwa wananchi wa Wilaya ya Same wanataka wawe na uhakika kwamba kweli kazi hii inafanyika, je, Serikali iko tayari kunisaidia nipate andiko hili la usanifu wa kina ili niweze kuwa na ushahidi kwamba kweli kazi hii itakwenda kufanyika? Ahsante. (Makofi)
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama tulivyoeleza katika jibu la msingi kwamba kazi hii imepangwa kufanyika katika robo ya nne ya mwaka huu wa fedha, tunaendelea kumwambia Mheshimiwa Mbunge aendelee kuwa na subira. Wizara inaendelea kupambana kuona namna ambavyo tunakamilisha kazi hii na kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kuondokana na changamoto hii.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tunataka tuwaridhishe wananchi ambao ndio wanapata changamoto kubwa ya kuenea na kuwepo kwa tope katika bwawa hili, na kwa kuwa tunataka tumpatie nafasi Mheshimiwa Mbunge cha kwenda kuzungumza kwa wananchi, tupo tayari na tutampatia hayo maelezo au hiyo taarifa ili naye aweze kujiridhisha na kazi iweze kuendelea, nakushukuru.
Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa tope lililojaa katika Bwawa la Kalemawe – Same?
Supplementary Question 2
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Hili swali limeulizwa hapa Bungeni mara nyingi sana, na majibu yanayotolewa na Serikali ni haya haya. Naomba nimwambie Mheshimiwa Waziri kitu kimoja, naomba leo anambie ni lini atakwenda kuliona lile Bwawa la Kalemawe ili wananchi waamini kwamba Serikali iko serious? Ahsante.
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mama Anne Kilango kwa kumwahidi kwamba mara tu baada ya kukamilika kwa Bunge hili, nitahakikisha kwamba tunafuatana pamoja kwenda katika hilo eneo ili kuona changamoto na kuona namna ambavyo tunaweza tukawasaidia wananchi wa eneo hilo, nashukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved