Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 4 | Enviroment | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 57 | 2025-01-31 |
Name
Constantine John Kanyasu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Geita Mjini
Primary Question
MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: -
Je, Serikali inafahamu ongezeko la magugu maji Ziwa Victoria na zipi athari za Magugu hayo na mpango wa kuyadhibiti?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafahamu ongezeko la magugu maji katika Ziwa Victoria ambayo yanasababisha athari za kimazingira, kiuchumi na kijamii ikiwemo kupungua kwa oksijeni kwenye maji ambayo huzuia mzunguko wa hewa na mwanga wa jua na hii husababisha vifo vya samaki na viumbe wengine wa majini. Uharibifu wa mifumo ikolojia na bioanuai ya Ziwa Victoria, huathiri maeneo ya mazalia ya samaki, shughuli za uvuvi na usafirishaji.
Mheshimiwa Spika, Serikali imechukua jitihada mbalimbali kuhakikisha inadhibiti magugu maji katika Ziwa Victoria ikiwemo kuandaa na kutekeleza Mkakati na Mpango Kazi wa Taifa wa Kukabiliana na Viumbe Vamizi wa Mwaka 2019/2029 ambao unatoa mwongozo wa namna ya kuzuia, kuingia na kuenea kwa viumbe vamizi na una mipango endelevu ya kushughulikia viumbe vamizi waliopo na wale wanaoweza kuingia.
Mheshimiwa Spika, aidha, kutoa elimu na kuwajengea uwezo wananchi wanaoishi karibu na Ziwa namna ya kujitolea katika kazi za kutokomeza na kuenea kwa magugu maji kila yanapojitokeza, ikiwa ni pamoja na kung’oa, kukausha na kuchoma magugu maji; na kuendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kudhibiti uharibifu wa mifumo ikolojia ndani ya Ziwa Victoria, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved