Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Enviroment Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 58 2025-01-31

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka Sheria kabambe kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti uharibifu wa mazingira na kutatua changamoto mbalimbali za kimazingira nchini, Serikali imetunga na inatekeleza Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura ya 191 ambayo inasimamia masuala yote yanayohusiana na mazingira nchini Tanzania. Sheria hii imeweka msisitizo wa udhibiti wa uharibifu wa mazingira kwa kukataza uchafuzi wa maji, hewa, na udongo kupitia kemikali za viwandani, kilimo, na shughuli nyingine za kibinadamu.

Mheshimiwa Spika, aidha, imeweka msisitizo kwa miradi yote mikubwa kwamba ni lazima ifanyiwe tathmini ya awali ya athari za mazingira kabla ya mradi kuanza ili kuepuka uharibifu wa mazingira. Pia, sheria inahimiza wananchi kuhamasishwa kushiriki katika uhifadhi na usimamizi kupitia elimu, sheria ndogo ndogo za Serikali za Mitaa, na mipango ya uhifadhi wa mazingira, nashukuru.