Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 59 2025-01-31

Name

Bonnah Ladislaus Kamoli

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Segerea

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza:-

Je, hatua gani za kinidhamu zimechukuliwa kwa madaktari wanaoendelea kuzuia Maiti kutokana na deni la matibabu kinyume na maelekezo ya Serikali?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, maiti huwa zinazuiliwa na uongozi wa hospitali zetu na wala siyo suala la madaktari. Katika maeneo ambayo tumefanya ufuatiliaji ili kuchukua hatua za kinidhamu kwa viongozi husika, tumebaini ndugu wa marehemu ndio waliokataa kufuata utaratibu uliowekwa kwa nia ya kuzuia hoja za ukaguzi. Badala yake, ndugu hao walikimbilia kulalamika kwenye vyombo vya habari na kwa viongozi, hasa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali ilishatoa maelekezo kwa vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini kupitia Waraka Na. 1 wa Mwaka 2021 wa kutozuia maiti na kuweka utaratibu wa kulipia gharama za matibabu na madeni ya miili.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.