Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 60 2025-01-31

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza: -

Je, watoto wa kike wangapi na wanawake wangapi walioathirika na utoaji mimba usio salama nchini?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2024 idadi ya wanawake na wasichana waliopata changamoto ya kuharibikiwa na mimba na kupata huduma katika vituo vya huduma za afya ni kama ifuatavyo: -

(i) Wanawake na wasichana 181,071 ambao walipatiwa huduma na kuruhusiwa kama wagonjwa wa nje (outpatients);

(ii) Wanawake na wasichana 32,512 ambao walipatiwa huduma wakiwa wamelazwa (inpatients).

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2024, wanawake 92 walipoteza maisha kutokana na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na kuharibika kwa mimba.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.