Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Finance and Planning Wizara ya Fedha 61 2025-01-31

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha jamii inapata uelewa kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na utoaji wa risiti za mauzo na ununuzi wa bidhaa na huduma. Hatua zinazochukuliwa na Serikali ni pamoja na: -

(i) Kutoa elimu elimu ya kodi kwa njia mbalimbali ikiwemo redio, runinga, mitandao ya kijamii, makongamano, maonesho ya biashara ya Kitaifa, Kimataifa na semina;

(ii) Kuwatembelea wafanyabiashara katika maeneo yao mlango kwa mlango, kutoa elimu inayoainisha wajibu wa mlipakodi kwa TRA na wajibu wa TRA kwa mlipakodi kupitia mkataba wa huduma kwa mlipakodi;

(iii) Kuanzisha huduma za bure ikiwemo namba za simu za bure zinazowezesha walipakodi kuwasiliana na Ofisi za TRA moja kwa moja; na

(iv) Kuanzisha ofisi zinazotembea (Mobile Tax Offices) ambazo zinatumika kama ofisi kamili kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi kwa umma na kusajili walipakodi wapya, ahsante.