Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Janeth Elias Mahawanga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha jamii inapata uelewa kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti?
Supplementary Question 1
MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Ni kwa kiasi gani Serikali inatumia teknolojia kusaidia ufuatiliaji wa ulipaji kodi na kudhibiti ukwepaji kodi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kuna mpango gani wa kuboresha mfumo wa utoaji risiti kwa kutumia teknolojia rahisi kwa wajasiriamali wadogo?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Janeth kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Janeth kwa namna anavyohamasisha na kutoa elimu kwa walipa kodi ili nchi yetu ama wananchi washiriki katika kulipa kodi bila shuruti. Pili, naomba uridhie maswali yote mawili niyajibu kwa pamoja.
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuimarisha mifumo ya mlipa kodi na kudhibiti mapato ya Serikali. Serikali imeweka msisitizo kuhakikisha kwamba mifumo yote inasomana na siyo tu kusomana, lakini kufanya mifumo iwe rafiki kwa mlipa kodi. Kwa mfano, leo Serikali kupitia TRA inatumia VFD (Virtual Fiscal Devices) ambayo mfanyabiashara anaweza kutoa risiti kupitia simu yake ya mkononi. Kwa sababu ya mifumo hiyo kuimarishwa, ndiyo tumeona siku hadi siku mapato yanaongezeka kwa kiasi kikubwa sana, ahsante sana. (Makofi)
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha jamii inapata uelewa kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti?
Supplementary Question 2
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na jitihada mbalimbali za Serikali kuiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hatimaye inafanya vizuri, lakini bado ipo mipaka ambayo haina scanner. Je, Serikali ina mpango gani kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kuiwezesha TRA fedha ili iweze kununua scanner kwenye mipaka mfano Namanga, Horohoro na Holili? Ahsante sana (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Subira ambaye ni Balozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Ni kweli anachokisema Mheshimiwa Mbunge, lakini Serikali imetenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa midaki mbalimbali (cargo) na midaki ya vifurushi vidogo vidogo. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba mwaka huu wa fedha tutanunua midaki sita na itasambazwa katika maeneo yote aliyoyataja. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved