Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Energy and Minerals Wizara ya Madini 63 2025-01-31

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza: -

Je, lini wananchi waliopisha mwekezaji katika Mgodi wa Shanta Kata ya Mang’onyi Jimbo la Singida Mashariki watalipwa fidia?

Name

Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Longido

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Shanta Mining Company Ltd ilianza shughuli za uzalishaji katika Mgodi wa Dhahabu Singida Machi, 2023 kwa leseni Na. 455/2012. Kabla ya kuanza shughuli za uzalishaji, jumla ya wananchi 284 walikuwa wameshalipwa fidia kwenye maeneo yao yenye ukubwa wa ekari 1,655 ambapo familia 26 zilizohamishwa zilijengewa makazi mapya ikiwemo miundombinu muhimu ya maji na barabara na kupewa ardhi yenye ukubwa wa ekari tano kila familia.

Mheshimiwa Spika, pia, jengo la taasisi ya kidini (Msikiti) lilihamishwa kwa kujengewa msikiti mpya. Jumla ya Shilingi za Kitanzania 4,353,897,083.00 zilitumika kabla ya kuanza shughuli za uzalishaji kwenye eneo hilo kwa ajili ya fidia ya ardhi na maendelezo yake pamoja na gharama za ujenzi wa makazi mapya.

Mheshimiwa Spika, zoezi la utwaaji wa ardhi kwenye leseni Na. ML 456/2012 na ML 457/2012 kwa ajili ya upanuzi wa shughuli za uchimbaji lilianza mwezi Agosti, 2024 na linaendelea katika hatua ya uthamini na ulipaji fidia ambapo zoezi la ulipaji fidia limeanza mwezi Januari mwaka huu wa 2025 na linaendelea kwa yale maeneo ambayo taarifa za uthamini zimeidhinishwa na Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuhakikisha zoezi la uthaminishaji katika maeneo yote husika linakamilika mapema na kulipa fidia kwa wahusika pamoja na kuzihamisha familia zinazoguswa na shughuli za uchimbaji. Ahsante sana.