Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 64 2025-01-31

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kuzuia usajili holela wa laini za simu mitaani kutokana na utapeli unaoendelea mitandaoni?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka miongozo ya kusajili laini za simu kupitia Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta. Miongozo hii inahakikisha kuwa laini zote zinasajiliwa kwa alama za vidole, hivyo kutokuwepo kwa mianya ya kusajili laini kiholela. Hata hivyo, wahalifu wa mtandaoni hutumia mbinu kwa kuwalaghai mawakala na watumiaji ili laini zilizokwishasajiliwa zitumike kwenye uhalifu.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TCRA na watoa huduma za mawasiliano inaendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu kupitia njia zifuatazo: -

(i) Kutoa elimu kwa umma juu ya uhalifu mtandaoni na njia za kujilinda;

(ii) Kuhakiki taarifa za usajili kupitia namba *106#; na

(iii) Kutoa taarifa za uhalifu kupitia namba 15040, ili kuchukua hatua stahiki dhidi ya vitendo vya udanganyifu.