Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 65 2025-01-31

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:-

Je, Serikali haioni kuwa uwepo wa aina nyingi za viuatilifu kwenye zao la korosho ni kuwachanganya wakulima?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, viuatilifu mbalimbali vimeidhinishwa katika kudhibiti visumbufu vya zao la korosho kulingana na aina za magonjwa yanayoathiri mimea. Viuatilifu hivyo, vimesajiliwa kwa majina tofauti ya kibiashara bila kuathiri viambata amilifu (Active Ingredients) vyenye uwezo wa kudhibiti vimelea na wadudu waharibifu katika zao hilo. Hivyo, zao la korosho linaonekana kuwa na viuatilifu vingi kutokana na majina ya kibiashara yanayotumika katika usajili.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania, TARI Naliendele, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Sekretarieti za Mikoa na wasambazaji wa viuatilifu imeendelea kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa viuatilifu, Maafisa Ugani na wakulima kuhusu matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, uhifadhi pamoja na viwango vya uzimuaji (Pesticide application rate), ili kuwezesha ufanisi wa viuatilifu vinavyosambazwa kwa wakulima.