Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 66 2025-01-31

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji, Ifumbo, Chunya?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Katika Mpango na Bajeti ya Mwaka 2025/2026 Serikali, kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, itatenga fedha, kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, ili kujua gharama halisi za ujenzi wa Skimu ya Ifumbo. Kazi hii ikikamilika taratibu za manunuzi za kumpata mkandarasi, kwa ajili ya ujenzi wa skimu hizi zitafuata.