Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Masache Njelu Kasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lupa
Primary Question
MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji, Ifumbo, Chunya?
Supplementary Question 1
MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Skimu ya Ifumbo ni ya muda mrefu na ilianza toka Serikali ya Awamu ya Nne. Serikali ya Awamu ya Nne ilitoa fedha na mradi huu ulianza, lakini haukufika mwisho. Kwa hiyo, kwa sababu, majibu ya Serikali yanasema itafanya tena upembuzi. Ni lini upembuzi huu utakamilika ili skimu hii iweze kukamilika na iweze kunufaisha wananchi wa Chunya?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kupitia mapato ya ndani ya halmashauri, tumeweza kufanya upembuzi wa awali na kuweza kugundua mabonde manne mazuri yanayofaa kujenga skimu ambayo inapatikana maeneo ya Sipa, Mafyeko, Luwalage, pamoja na Mkola. Hivyo, tumeandika andiko kuleta Wizarani na kuweza kuomba fedha, kwa ajili ya upembuzi wa kina. Ni lini Serikali itatupatia fedha hizi ili upembuzi wa kina uweze kufanyika? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge Masache Njelu Kasaka kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo lake la Lupa. Nimthibitishie tu kwamba, kwanza tumepanga katika mwaka wa fedha unaokuja 2025/2026, upembuzi yakinifu utamilika kwa sababu jambo hili tumeshalipa kipaumbele. Kwa hiyo, aondoe shaka, litakamilika na tutahakikisha tunamtangaza mkandarasi ili liweze kufanyiwa kazi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu fedha ambazo wameziomba kwenye maeneo hayo manne, nimeongea na Mkurugenzi wa Tume na amenihakikishia kwamba, tumeweka kwenye bajeti hii inayokuja, yaani lipo ndani ya bajeti. Kwa hiyo, tukishamaliza kupitisha bajeti, maana yake ni sisi kudhibiti hizo fedha ili sasa tukamalize hiyo kazi ili wananchi wake waweze kunufaika na miradi yote ambayo halmashauri imekusudia, ahsante.
Name
Edward Olelekaita Kisau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kiteto
Primary Question
MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji, Ifumbo, Chunya?
Supplementary Question 2
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Mradi wa Umwagiliaji wa Ngiba ya Ngusero ulishakuwa kwenye bajeti iliyopita. Mradi huo unaanza lini? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli tuko kwenye hatua za mwisho, kama Mheshimiwa Mbunge alivyokuwa ameeleza. Tukishamaliza tu, maana yake tutamkabidhi Mkandarasi site ili aweze kufanya kazi. Kwa hiyo, tuko kwenye hatua za mwisho na anafahamu utaratibu wa kazi jinsi Serikali ambavyo tunafanya. Ahsante.
Name
Ally Anyigulile Jumbe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyela
Primary Question
MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji, Ifumbo, Chunya?
Supplementary Question 3
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ni lini Skimu ya Umwagiliaji ya Makware itaanza kufanya kazi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, natambua kazi nzuri inayofanyika pale Kyela. Kuhusu Mradi wa Makwale na wenyewe tumeshautangaza ili kuhakikisha tunapata Mkandarasi uweze kufanyiwa kazi. Kwa hiyo, tukae tu mkao tayari, kwani baada ya Bunge kwisha, ninaamini miradi yote ambayo Serikali ilikuwa imepanga kuitekeleza itakuwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake ili sasa wananchi waweze kupata matunda kutokana na kazi ya Daktari Samia Suluhu Hassan. Ahsante.
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji, Ifumbo, Chunya?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, Skimu ya Mawala, Skimu ya Soko na Kimanga Mau, pale kwenye Kata ya Kahe Magharibi na Mashariki zimetengewa fedha kwenye Bajeti ya 2023 na 2024 zile fedha hazikuja na kwa hiyo, ukarabati haukufanyika. Pia, kwenye mwaka 2024/2025 mpaka sasa hivi afisa mhusika anasema iko kwenye ngazi ya manunuzi. Je, itakamilika lini ili tuweze kupata ukarabati wa skimu hizi? Ahsante sana.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, Kama alivyouliza Mheshimiwa Kimei, Mbunge wa Vunjo, ni kweli skimu zote alizozitaja ziko katika hatua ya manunuzi. Hatua za manunuzi ni mchakato. Tukishamaliza mchakato wa manunuzi, tunapeleka katika hatua inayofuata ya kufanya vetting kupitia Ofisi ya CAG.
Mheshimiwa Spika, baada ya kumaliza vetting, ndiyo tutakwenda katika hatua ya mwisho ya kumkabidhi mkandarasi site. Kwa hiyo, kwa sababu ni taratibu, Bunge liliziweka nasi inabidi tuzifuate ili tuweze kukamilisha. Kwa hiyo, tukimaliza hizi taratibu ambazo zina muda wake, maana yake miradi hii itakwenda kukamilika. Kikubwa ni kwamba, ziko kwenye mchakato wa ukamilikaji ili ziweze kufuata sheria. Kwa hiyo, hili litafanyika, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved