Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 67 2025-01-31

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ahadi yake ya kutenga maeneo maalum ya biashara kwenye Eneo la NDC, Kiwanda cha KMTC, Njiapanda ya Machame?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Mpango Mkakati wa matumizi ya eneo la KMTC chini ya NDC ulikuwa ni kujengwa viwanda mbalimbali, makazi ya wafanyakazi wa viwanda na mahitaji mengine. Kwa sasa, kimejengwa Kiwanda cha Kuzalisha Mashine na Vipuri cha KMTC kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 16.

Mheshimiwa Spika, eneo lenye ukubwa wa jumla ya ekari 639 linaandaliwa mpango wa uwekezaji, kwa ajili ya kujenga mji wa viwanda (Smart Industrial City). Mpango huo umewekwa katika Vipaumbele vya Mwaka wa Fedha 2025/2026 vya Sekta ya Viwanda na Biashara, ambapo utahusisha ujenzi wa miundombinu ya msingi ikiwemo barabara, mifumo ya majisafi na majitaka, umeme na industrial shades ambapo kukamilika kwake kutawezesha uanzishwaji wa viwanda vingine, ahsante