Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ahadi yake ya kutenga maeneo maalum ya biashara kwenye Eneo la NDC, Kiwanda cha KMTC, Njiapanda ya Machame?

Supplementary Question 1

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Pamoja na mpango huo mzuri wa kujenga viwanda na miundombinu mingine kutokana na adha kubwa wanayopata wananchi wa Ukanda wa Machame kwenda kufuata bidhaa Moshi Mjini au maeneo mengine, je, Serikali haioni iko haja ya kuweka mji mdogo wa kibiashara ambao bidhaa na vitu vingine vitapatikana Njiapanda ya Machame?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Serikali iliahidi kukamilisha ujenzi wa Kiwanda cha Losaa, ili kianze kutoa huduma. Je, ni lini ujenzi na ukamilishaji wa kiwanda hiki utakamilika?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Saashisha Mafuwe kwa ufatiliaji wa maendeleo ya viwanda katika Jimbo lake la Hai, hasa hilo mahususi la Machame.

Mheshimiwa Spika, ni kweli amekuwa akifatilia kwa umuhimu wa mji huu mdogo ambao unatakiwa kuwa na maeneo ya kufanya biashara ambao upo karibu na eneo la KMTC. Kama nilivyosema, Serikali tayari imeshaweka masterplan, tumeshamnunua Mshauri Mwelekezi, City Plan Consultant Ltd, ambaye atapanga vizuri eneo hili ambalo Mheshimiwa Mbunge anataka kwa ajili ya eneo la biashara na tumeshakubaliana tutapanga, ili tuone eneo hilo linakuwa na maeneo ya makazi na huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo maeneo ya kufanyia biashara ambayo ndiyo hasa, lengo la Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, nikuhakikishie, katika Mji Mdogo wa Machame kutakuwa na maeneo ya biashara vikiwemo vituo vya mafuta, nakadhalika, ambavyo vitasaidia wananchi wa pale kuweza kupata maeneo ya kufanya biashara katika eneo hilo la KMTC.

Mheshimiwa Spika, kuhusu eneo la pili la Kiwanda cha Losaa. Tayari Serikali, kupitia Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo vidogo (SIDO), tumeshaweka kwenye bajeti ya mwaka huu. Tutapanga mwaka huu ili kwenda kukiendeleza kile kiwanda kidogo, wananchi wa Losaa waweze kunufaika na uwepo wa kiwanda hicho. Nakushukuru.