Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 7 2025-01-28

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:-

Je, lini Serikali itaondoa usumbufu wa kupata vibali na gharama pale raia wa Tanzania wanapolazimika kushiriki shughuli za kijamii Nchini Zambia?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imefunga mifumo ya kielektroniki katika ngazi za Mikoa na Wilaya ili kurahisisha upatikanaji wa hati za safari (pasipoti) na hati za dharura za safari kwa lengo la kuwaondolea usumbufu raia wa Tanzania pale wanapohitaji hati hizo kwa ajili ya kushiriki shughuli za kijamii katika nchi jirani. Kwa raia wanaoishi ndani ya eneo lisilozidi kilometa 10 kutoka mpaka wa nchi yetu na nchi jirani na wananchi wanapokuwa na shughuli za dharura kama vile misiba na magonjwa, hupatiwa ruhusa maalum kuwawezesha kwenda umbali usiozidi kilomita 10 ili waweze kushiriki shughuli hizo.

Mheshimiwa Spika, aidha, kwa wale wanaoenda nchi jirani kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, wanapaswa kufuata sheria na taratibu za nchi husika katika kulipia vibali vinavyoendana na shughuli wanazoenda kufanya. Ahsante.