Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, lini Serikali itaondoa usumbufu wa kupata vibali na gharama pale raia wa Tanzania wanapolazimika kushiriki shughuli za kijamii Nchini Zambia?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninaomba niulize maswali madogo kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa mwananchi wa kawaida ambaye anaenda kushiriki shughuli za kijamii kutozwa kibali shilingi 20,000 ni gharama kubwa sana. Je, Serikali itakuwa tayari kupunguza tozo hizo ili walau iwe shilingi 5,000 au shilingi 2,000 ikiwezekana?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; ninashukuru Serikali wamefunga vifaa vya kielektroniki, ninataka kujua katika Wilaya ambazo zimenufaika na Wilaya ya Kalambo ni miongoni mwao? Ahsante sana.

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali ya Mheshimiwa Kandege, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tozo hizi za shilingi 20,000 zipo kwa mijibu wa sheria pale ambapo tutaona kuna haja ya kupunguza basi Serikali itayafanyia kazi mapendekezo ya Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, nadhani ameipongeza Serikali kuweka mifumo ya kielektroniki ambapo Wilaya ya Kalambo pia imenufaika. Ahsante sana.