Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 9 2025-01-28

Name

Iddi Kassim Iddi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Makao Makuu ya Polisi katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ina kituo cha polisi daraja B ambacho kinakidhi mahitaji ya kutoa huduma ya polisi kwa wananchi wa Msalala. Kituo hiki kipo eneo la Bugarama na kina miundombinu yote ya msingi ikiwemo Ofisi za Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OC-CID), Mkuu wa Kituo (OCS), Ofisi ya Makosa ya Usalama Barabarani pamoja na Ofisi ya Dawati la Kushughulikia Ukatili wa Kijinsia. Kituo hiki kitatumika kama Makao Makuu ya Polisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kahama. Ahsante.