Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Makao Makuu ya Polisi katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama?

Supplementary Question 1

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Iddi Kassim, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Swali la kwanza; Serikali iliahidi kujenga nyumba za watumishi wa Jeshi la Polisi pamoja na viongozi katika Wilaya ya Hai; je, ni lini Serikali itaanza kujenga nyumba hizi za watumishi?

Swali la pili; kwa kuwa wamesema pale Msalala ni makao makuu, je, hawaoni kuwa ipo haja ya kujenga nyumba za watumishi?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza, ya Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kuna upungufu wa nyumba za watumishi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Wilaya ya Hai na Wilaya ya Msalala kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, nyumba hizi tunazijenga kwa awamu. Kwa hiyo, nimhakikishie Mbunge kwamba tutaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga nyumba za watumishi wetu ambao ni askari katika maeneo ya Hai pamoja na Msalala kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante sana.