Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 11 2025-01-28

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga mnara wa simu katika Kata ya Kerebe Muleba?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidigitali wa Awamu ya Kwanza (DTP) ambapo mkataba wake ulisainiwa tarehe 13 Mei, 2023 na utekelezaji unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 12 Mei, 2025. Kupitia mradi huu Kata ya Kerebe imejumuishwa na kupata mtoa huduma wa Vodacom.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mnara huu wa Vodacom katika Kata ya Kerebe upo katika hatua za awali ambapo mtoa huduma ameanza uchimbaji wa msingi na ujenzi wa mnara huu. Aidha mnara huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari 2025. Hivyo, kukamilika kwa mradi huu kutaboresha huduma za mawasiliano ya simu katika kata hiyo, ambapo mnara huu umelenga kunufaisha Kijiji cha Makibwa na vijiji vingine vya jirani.