Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Oliver Daniel Semuguruka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga mnara wa simu katika Kata ya Kerebe Muleba?
Supplementary Question 1
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninayo maswali mawili ya nyongeza. Ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; je, ni lini sasa Serikali itasimamia wanaojenga minara hii ya ziwani waweze kuweka taa kwa ajili ya kuwamulikia wale wavuvi wote wanaosafiri wakati wa usiku ziwani katika visiwa vyote vya Wilaya ya Muleba?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, ni lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Nterungwe Kamata ya Nyamiaga katika Jimbo la Ngara ambapo hakuna mawasiliano kabisa?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Oliver Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, suala la kuweka taa kwenye minara ninapenda kusema kwamba nimelipokea. Tayari kuna baadhi ya maeneo tulipewa maombi hayo na tukafanya, basi naahidi na eneo hili pia tutalizingatia.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa suala la kata hii aliyoitaja, kuhusiana na ujenzi wa mnara katika eneo hili la Ngara tutaendelea pia kuweka makadirio ya kuhakikisha maeneo yote ambayo minara bado haijajengwa, inajengwa na kuboresha hali ya mawasiliano maeneo yote nchini. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved