Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Water and Irrigation Wizara ya Maji 12 2025-01-28

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza:-

Je, Mradi wa Kutoa Maji Ziwa Tanganyika ili kumaliza changamoto ya maji Nkasi umefikia wapi?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mkakati wa kutoa maji Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji katika Mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa ikiwemo Wilaya ya Nkasi. Serikali kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za kumpata mtaalam mshauri kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa mradi huo ambapo unatarajiwa kuanza mwezi Aprili, 2025.