Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Aida Joseph Khenani
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza:- Je, Mradi wa Kutoa Maji Ziwa Tanganyika ili kumaliza changamoto ya maji Nkasi umefikia wapi?
Supplementary Question 1
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, ninatambua jitihada za Serikali kwenye jambo hili muhimu, lakini majibu ya Serikali wanasema mwezi Aprili mwaka huu ndio wanategemea angalau hatua za usanifu wa kina zitaanza. Swali la kwanza; je, wana mpango mkakati gani kwa kipindi hiki wa kuleta mradi wa muda mfupi wakati tunasubiri mradi huo wa muda mrefu?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; pamoja na kwamba ni mradi ambao utatumia gharama kubwa, Mamlaka ya Mji Mdogo Namanyere upatikanaji wa maji ni 49% huku upotevu wa maji ni ukiwa ni 43%; ni asilimia sita tu ndiyo inayowafikia wananchi, na tunahitaji shilingi bilioni 1.8; je, ni lini wataleta fedha hizo kabla ya kuleta Mradi huo mrefu wa Kutoa Maji Ziwa Tanganyika?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninatambua na Serikali pia inatambua changamoto ya maji na imekuwa na mkakati wa muda mfupi, wa kati na mrefu. Tunatambua Mheshimiwa Aida anawasilisha changamoto ya wananchi wake; lakini Serikali ina mkakati na programu ya visima 900 ambapo tunaendelea navyo. Kwa upande Mheshimiwa Aida tuna upande wa Ninde, Kipili pamoja na Isale Group kuna mradi huo wa vijiji sita, pamoja na Paramawe.
Mheshimiwa Spika, tunaamini kabisa kwamba huu ni mkakati ambao utasaidia kutatua changamoto kwa kipindi ambacho tunaendelea na utekelezaji wa mradi wa muda mrefu.
Mheshimiwa Spika, vilevile Serikali inatambua upotevu wa maji katika mji mdogo; na hii ni kwa sababu ya miundombinu kuwa chakavu. Sasa Serikali tulitenga kiasi cha shilingi milioni 815 ambazo zitashughulikia miundombinu na kurekebisha maeneo ambayo miundombinu yake imechakaa ili kuhakikisha kwamba tunaondoa upotevu wa maji kutoka 43% kwenda katika 25% inayokubalika kimataifa. Ahsante.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza:- Je, Mradi wa Kutoa Maji Ziwa Tanganyika ili kumaliza changamoto ya maji Nkasi umefikia wapi?
Supplementary Question 2
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itatoa maji Ziwa Victoria kupitia Mradi wa Mugango – Kiabakari – Butiama kuja Nyamuswa na kusamba Jimbo Zima la Bunda?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mradi kutoka Mugango – Kiabakari tayari umekwishakamilika 100% na wananchi wanapata huduma ya maji kutoka Butiama. Kuhusiana na kupeleka upande wa Nyamuswa tumesanifu mradi wa shilingi bilioni nane na tayari mkandarasi ameshapatikana. Tunatarajia ifikapo mwezi Februari mkandarasi ataanza kazi mara moja. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved