Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 14 2025-01-28

Name

Mrisho Mashaka Gambo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arusha Mjini

Primary Question

MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:-

Je Serikali ina mpango gani wa kuingia ubia na Hospitali ya ALMC Arusha ili kuiokoa na changamoto za kifedha zinazoikabili?

Name

Jenista Joackim Mhagama

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Peramiho

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI K.n.y. WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ninaomba nijibu swali la Mheshimiwa Mrisho Gambo, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa sasa mchango wa Serikali katika Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre unatolewa katika huduma za chanjo, huduma za VVU (miradi msonge), kifua kikuu pamoja na fedha za bidhaa za afya ambapo kwa mwaka kiasi cha shilingi milioni 536.8 kimetolewa.

Mheshimiwa Spika, Serikali ilishaanza kufanyia kazi ombi la Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre kwa lengo la kuhakikisha inakamilisha mkataba wa makubaliano ya ubia kati ya Serikali na hospitali hiyo ili kuiwezesha kutoa huduma bora na endelevu.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali inachangia kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya malipo ya mishahara, fedha za dawa na vifaa tiba pamoja fedha za matumizi mengineyo katika Hospitali ya Seriani ambayo pia inamilikiwa na Kanisa la KKKT – Arusha.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.