Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 1 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 17 | 2025-01-28 |
Name
Mariamu Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA I. ALEX K.n.y MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuliendeleza Pori la Pande lililopo Dar es salaam kuwa kivutio cha Utalii?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-
Mheshimiwa Spika, pori la akiba la Pande ni pori pekee lililopo katika Jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya misitu ya Ukanda wa Pwani. Kuanzia Mwaka wa Fedha 2021/2022, Wizara ilijenga miundombinu mikubwa ya maeneo ya kupumzikia wageni na kambi za watalii katika eneo hilo. Vilevile, mwaka 2023/2024 Wizara imeanzisha bustani ya wanyamapori na kuweka wanyama katika eneo hilo ambapo mpaka sasa, pori hilo lina idadi ya wanyama zaidi ya 100. Aina za wanyama waliopo sasa ni duma, mamba, simba, pundamilia, nyumbu, swala granti, swala pala na nyoka wa aina mbalimbali akiwemo chatu.
Mheshimiwa Spika, sambamba na hatua hizo, miundombinu ya barabara katika pori hilo imeboreshwa na inapitika katika kipindi chote cha mwaka na Wizara imejenga lango kuu la kuingilia kwenye pori hilo. Kufuatia juhudi hizo, idadi ya watalii wanaotembelea pori hilo imeendelea kuongezeka ambapo kuanzia mwaka 2023 hadi 2024 watalii 4,606 wameweza kutembelea. Aidha, Wizara imetenga maeneo mahususi kwa ajili ya uwekezaji katika miundombinu ya michezo ya watoto yenye kiwango cha kimataifa pamoja na huduma za malazi. Hivyo, wawekezaji wanakaribishwa kutumia fursa hii kuwekeza kwenye pori hilo kwa lengo la kukuza utalii.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved