Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA I. ALEX K.n.y MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuliendeleza Pori la Pande lililopo Dar es salaam kuwa kivutio cha Utalii?

Supplementary Question 1

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Spika, ninaipongeza Serikali kwa kazi kubwa ambayo imefanyika katika pori hili. Swali la kwanza; ni nini mkakati wa Serikali kuongeza wanyama katika pori hili?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; pia, kwenye jibu la msingi imeeleza tu kwamba uwekezaji uliopo sasa hivi ni kwenye miundombinu ya michezo. Tunaomba kufahamu kama kuna uwekezaji mwingine ambao unapatikana katika pori hili? Ahsante. (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba idadi inaonekana ni ndogo, lakini tuna mpango wa kuongeza wanyama kwenye eneo hili. Tutakuwa tunaongeza taratibu kulingana na ikolojia ilipo na uwezo wa kuhimili wanyama hao kupokelewa. Pia, kwenye eneo la uwekezaji tumesema kwamba ukiacha kuwekeza kwenye viwanja vilevile tunatoa fursa kwenye kuwekeza maeneo ya malazi ndani ya eneo hili.