Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Finance and Planning Wizara ya Fedha 18 2025-01-28

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BERNADETA K. MUSHASHU aliuliza:-

Je, lini Serikali itawalipa wateja walioweka fedha zao katika Kagera Cooperative Bank?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Januari 4, 2018, Benki Kuu ya Tanzania iliifutia leseni ya biashara benki ya wakulima Mkoa wa Kagera na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana kuwa mfilisi wa benki hiyo. Hadi Desemba 2024, jumla ya shilingi milioni 846.16 kati ya shilingi milioni 899.56 sawa na 94.06% zilimelipwa kama fidia ya bima ya amana kwa wateja 1,391 waliojitokeza kati ya wateja 2,797 waliokuwa na amana isiyozidi shilingi 1,500,000. Aidha, katika kipindi hicho, Bodi ya Amana imelipa wadai wa benki fidia ya ufilisi shilingi milioni 664.25 kati ya madai ya shilingi bilioni 1.64 sawa na 40.50% kwa wateja 195 kati ya wateja 274 wanaostahiki kulipwa fidia hiyo.

Mheshimiwa Spika, ninatoa rai kwa Mheshimiwa Mbunge, tuendelee kuhamasisha wananchi wanaodai fedha zao kuwasiliana na Bodi ya Bima ya Amana ili kulipwa stahiki zao.

Mheshimiwa Spika, ahsante.