Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Bernadeta Kasabago Mushashu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BERNADETA K. MUSHASHU aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa wateja walioweka fedha zao katika Kagera Cooperative Bank?
Supplementary Question 1
MHE. BERNADETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa ni miaka nane sasa tangu Benki ya Wakulima ya Kagera kufungwa, lakini waliokuwa na amana au fedha zaidi ya shilingi milioni moja na nusu wamelipwa 43% tu ya fedha walizokuwa wameweka benki, ni lini Serikali itawalipa watu hawa 57% ya fedha zao zilizobaki benki kwa sababu wanateseka?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa watumishi waliokuwa kwenye benki hiyo walilipwa nauli tu wakaahidiwa kulipwa stahiki zao, ni lini stahiki zao za kiutumishi zitalipwa kwa sababu hawajalipwa hata senti tano mpaka leo? (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu ninaomba kumpongeza sana kwa namna anavyofuatilia kwa karibu sana suala hili. Hii 40% ambayo tumefika kuna mchango wake mkubwa sana pamoja na Waheshimiwa Wabunge wengine.
Mheshimiwa Spika, malipo yanaendelea kulipwa na dirisha bado halijafungwa. Kwa hiyo tuendelee kuhamasisha watu wetu wadai, wawasiliane na Bodi ya Bima ya Amana ili kulipwa madai yao. Kuhusu watumishi, haya ni masuala ya kiutumishi. Ninaomba hili tulichukue nikae naye na watu wetu wa utumishi ili tuweze kuwasaidia watumishi wetu hawa. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved