Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Mifugo 19 2025-01-28

Name

Kilumbe Shabani Ng'enda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha maboresho ya Kanuni za Uvuvi ili kupata ufumbuzi wa aina ya wavu wa kuvulia samaki aina ya migebuka?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa ikifanya maboresho katika Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009. Aidha, Kanuni hizi zimekuwa zikiboreshwa kila mara ambapo mwaka 2018, 2019, 2020 na 2022 maboresho yalifanyika ili kukidhi mahitaji ya usimamizi na uendeshaji wa shughuli za uvuvi nchini. Hata hivyo, Wizara imekamilisha utaratibu wa kutoa Waraka wa Matumizi ya Wavu wa Makila kwa ajili ya uvuvi wa samaki aina ya migebuka katika Ziwa Tanganyika ambapo, Waraka huu utakuwa ni hatua za haraka na za awali katika kutatua changamoto inayowakabili wavuvi katika Ziwa Tanganyika.