Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kilumbe Shabani Ng'enda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha maboresho ya Kanuni za Uvuvi ili kupata ufumbuzi wa aina ya wavu wa kuvulia samaki aina ya migebuka?

Supplementary Question 1

MHE. KILUMBE S. NG’ENDA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mwaka 2022 maboresho yaliyofanyika katika Kanuni hizi za Uvuvi hayakugusa wavu huo unaovua samaki aina ya mgebuka na huyu ndiye samaki ambaye anapatikana kwa wingi katika Ziwa Tanganyika. Kwa muda wa miaka mitano tangu nimekaa katika Bunge hili tunazungumza Kanuni hii tu bila kufikia mwisho. Ni lini tutafikia mwisho wa suala la kupata kanuni inayoruhusu wavu wa kuvua samaki wa mgebuka na kanuni nyingine zinazohusu usalama katika Ziwa Tanganyika? (Makofi)

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, kwa sasa Waraka unakamilishwa na upo hatua za mwisho kwa ajili ya kuja kutatua tatizo hili ambalo linahusu wavuvi ambao wanahusika sana katika uvuvi wa samaki aina ya migebuka. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge, awe na matumaini jambo hili linaenda kutatuliwa hivi karibuni. Miaka mitano tuisahau sasa tuko kwenye kipindi cha utekelezaji.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha maboresho ya Kanuni za Uvuvi ili kupata ufumbuzi wa aina ya wavu wa kuvulia samaki aina ya migebuka?

Supplementary Question 2

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ipo tayari kuboresha kanuni za uvuvi ili 10% ya mapato ya Sekta ya Uvuvi yanayopaswa kurejeshwa kuendeleza sekta iweze kutekelezeka kama sheria inavyotaka ili wanawake wanaojihusisha na sekta hii waweze kuepuka changamoto wanazopitia kwa kutumia miundombinu isiyo rafiki wakati wa kwenda kununua samaki kama vile kujenga maeneo ya kununulia samaki kwenye mialo yetu?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, tunaendelea na matayarisho ya waraka na ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge muda mfupi ujao haya ambayo unayaeleza yanaenda kuwa katika muundo wa kimaandishi ili wananchi waweze kunufaika na utekelezaji wa zoezi la uvuvi.