Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 20 2025-01-28

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:-

Je, majosho mangapi yatajengwa katika Halmashauri ya Itigi katika Mwaka huu wa Fedha?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara ilijenga majosho saba yenye thamani ya shilingi 161,000,000 katika Kata ya Kitaraka yalijengwa majosho mawili, Mwamagembe josho moja, Idodyandole josho moja, Mitundu josho moja, Mtakuja josho moja na Majengo josho moja, katika Halmashauri ya Itigi. Aidha, Wizara itaendelea kuweka katika mpango wa bajeti ya mwaka 2025/2026, ujenzi wa majosho nchini yakiwemo majosho katika Halmashauri ya Itigi kulingana na upatikanaji wa fedha.