Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Je, majosho mangapi yatajengwa katika Halmashauri ya Itigi katika Mwaka huu wa Fedha?
Supplementary Question 1
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Serikali, ninaomba nijue kuhusu majosho Mbogwe; mwaka jana yalikuwepo kwenye bajeti na hata mwaka huu yapo. Ni lini sasa utekelezaji wake utafanywa ili majosho hayo ya Mbogwe yakamilike? (Makofi)
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Maganga. Mbogwe itakuwa miongoni mwa majosho yanayowekwa kwenye mpango wa bajeti ya 2025/2026. Mheshimiwa Mbunge, tuwe na subira kidogo tu, tutapata mahitaji haya.
Name
Nicholaus George Ngassa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igunga
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Je, majosho mangapi yatajengwa katika Halmashauri ya Itigi katika Mwaka huu wa Fedha?
Supplementary Question 2
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru. Jimbo la Igunga ni moja ya majimbo yenye mifugo mingi sana nchini. Je, ni lini Serikali itaanza kujenga majosho kwenye Kata za Mwamashiga, Mwamashimba na Mwamakona? Ahsante.
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyolieleza Bunge lako Tukufu katika swali la msingi ni kwamba tumeweka katika Mpango wa Bajeti inayokuja ya mwaka 2025/2026 kuendeleza ujenzi wa majosho yote hapa nchini yakiwepo majosho ya Mheshimiwa Ngassa kule Igunga.
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Je, majosho mangapi yatajengwa katika Halmashauri ya Itigi katika Mwaka huu wa Fedha?
Supplementary Question 3
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Ni lini Serikali itaanza ujenzi wa majosho manne ambayo yamekuwa yakitokea kila mwaka wa bajeti ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba? (Makofi)
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyojieleza kwenye jibu langu la msingi, tunaliweka kwenye makadirio ya fedha ya kipindi cha 2025/2026 ambapo tunakwenda kujenga majosho mengi kwa nchi nzima na jimbo la Chemba litakuwa sehemu ya mradi huo. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved