Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 6 2025-01-28

Name

Jafari Chege Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Primary Question

MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:-

Je, lini wizi wa mifugo utadhibitiwa Wilayani Rorya?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi lina wajibu wa kudhibiti wizi wa mifugo katika Wilaya ya Rorya. Jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi ni pamoja na kutoa elimu juu ya ulinzi jirani, kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi na mazizi salama. kuimarisha kikosi cha kupambana na wizi wa mifugo kwa kuongeza askari na vitendea kazi, kufanya mikutano ya ujirani mwema na Polisi Wilaya ya Nyatike ya Nchini Kenya juu ya udhibiti wa makosa yanayovuka mipaka na jitihada zote hizi ni endelevu na zimepunguza kwa kiasi kikubwa wizi wa mifugo. Aidha, takwimu zinaonesha katika kipindi cha mwezi Disemba, 2023 na mwezi Januari, 2024 kumeripotiwa matukio 26 na kipindi kama hicho mwezi Disemba, 2024 na mwezi Januari, 2025 kumeripotiwa matukio tisa, sawa na upungufu wa matukio 17. Ahsante.