Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jafari Chege Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Primary Question

MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:- Je, lini wizi wa mifugo utadhibitiwa Wilayani Rorya?

Supplementary Question 1

MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na jitihada hizi zinazofanywa na Jeshi la Polisi kudhibiti wizi wa mifugo, lakini bado wizi huu upo na unaathiri kwa kiasi kikubwa sana wananchi kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; ninataka nijue kama Serikali haioni sasa ni muda muafaka wa kuja na njia mbadala badala ya hizi zilizozoeleka ili kuweza kudhibiti wizi wa mifugo kwa sababu imechukua zaidi ya miaka 20 sasa kwenye eneo eneo lile?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwa changamoto kubwa ni pamoja na ukosefu wa vitendeakazi hasa magari ya doria. Je, Serikali haioni sasa ni muda muafaka wa kupeleka magari hasa kwa vituo vyote vitatu kwa maana ya Kinesi, Utegi na Shirati ili kuendelea kudhibiti wizi wa mifugo kwenye eneo lile?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Chege, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi kwa sasa njia ambayo tungependekeza ni kuimarisha ulinzi shirikishi pia kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wetu kuhusu suala zima la wizi wa mifugo katika eneo hili la Rorya.

Mheshimiwa Spika, kwa swali la pili kuhusu vitendeakazi, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Jeshi la Polisi limeagiza magari ya kutosha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inaimarisha ulinzi na usalama maeneo mbalimbali ikiwemo Wilaya ya Rorya. Ahsante sana.