Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 91 2025-02-04

Name

Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza: -

Je, Mstaafu aliyecheleweshewa kupata mafao, anaweza kudai fedha kutokana na usumbufu alioupata wakati anasubiri mafao yake?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PSSSF katika vifungu 49(3) na 43(3) mtawalia, vinaeleza kuwa endapo mfuko utachelewesha kulipa mafao kwa mwanachama na uchelewesho huo haukusababishwa na mwanachama mwenyewe au mwajiri, Mfuko utamlipa mwanachama huyo mafao yake pamoja na riba ya 15% kwa mwaka, ya kiasi atakachokuwa amelipwa kama mafao kwa Mfuko wa NSSF na asilimia tano kwa Mfuko wa PSSSF.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, sheria imetoa haki ya mwanachama kulipwa fidia endapo atacheleweshewa kulipwa mafao yake ikiwa ucheleweshaji huo umesababishwa na mfuko, ahsante.