Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Fakharia Shomar Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza: - Je, Mstaafu aliyecheleweshewa kupata mafao, anaweza kudai fedha kutokana na usumbufu alioupata wakati anasubiri mafao yake?
Supplementary Question 1
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na maelezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Maelezo yake yanaeleweka kwa sababu yeye amepita kwenye sheria, lakini nataka kujua ni sababu zipi za msingi ambazo mara nyingi huchelewesha watu kupata mafao yao kwa haraka? Ingawa sheria ipo, lakini kuna kitu hapo nimekwambia cha msingi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kawaida, Serikali inafahamu tarehe ya wastaafu wake. Je, hawa wanaohusika kufanya shughuli hizo za wastaafu tunawadhibiti vipi ili nao wasiwajibike, kwa sababu na wao ni sehemu ya kuwafanya wale wastaafu wachelewe? (Makofi)
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana kwa swali hilo zuri. Tayari Serikali imeshachukua hatua. Utakumbuka Bunge lako lililopita tulifanya mabadiliko kwenye hizi sheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa baada ya kutambua kwamba kulikuwa kuna changamoto zilizokuwa zinasababisha wastaafu kutokulipwa kwa wakati, moja ya changamoto ilikuwa kwamba, wanapoombwa nyaraka labda za tarehe ya kuajiriwa, lakini mwisho wanaombwa taarifa nyingine ambazo kimsingi mwajiri alipaswa kuwanazo; na upande wa mfuko pia, kulikuwa kuna changamoto za taarifa, na ukinzani wa taarifa. Hizi zilisababisha sana wastaafu hawa wakawa hawapati fedha zao kwa wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kubaini changamoto hizo pamoja na nyinginezo za kifedha na hali ya mifuko, tulileta mabadiliko ya sheria hapa. Tulitunga sheria na baadaye Bunge lako Tukufu lilipitisha mafao kwamba lazima yalipwe ndani ya siku 60 na ikiwa hayajalipwa ndani ya siku 60 ndiyo inatokea hiyo interest ya kulipwa 15% kwa asilimia tano.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika eneo la uwajibikaji. Tumekuwa na uwajibikaji mkubwa kwa sababu sheria hizi sasa tumekuwa tukizitekeleza kuhakikisha kwamba mfanyakazi ambaye kabla ya kustaafu kwake ndani ya miezi mitatu, taarifa zake zinatafutwa, zinahakikiwa na wakati unapokuja kufika analipwa. Hizo siku 60 tulizoziweka kwa mujibu wa sheria, mara nyingi hazitimii, wengine wanalipwa ndani ya siku tatu, ndani ya siku saba. Yaani siku 60 ni threshold ya mwisho kabisa ya utekelezaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumesha-advance kwenye Mfuko wa NSSF na PSSSF. Sasa tunatumia Mifumo ya TEHAMA na taarifa zinatolewa kiganjani kwa kutumia simu ya kiganjani (smartphone) kwa wafanyakazi ambao hata wale wanaolekea kustaafu. Kwa hiyo, taarifa zao za mifuko na michango zinatolewa kule. Kwa hiyo, hilo tatizo halipo tena, ahsante.
Name
Janejelly Ntate James
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza: - Je, Mstaafu aliyecheleweshewa kupata mafao, anaweza kudai fedha kutokana na usumbufu alioupata wakati anasubiri mafao yake?
Supplementary Question 2
MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona kwenye mifuko wameweka hiyo penalty. Sasa kwa Serikali mmeacha wazi, ni nini kinachosababisha kukae wazi? Napenda Serikali ituambie upande wa Serikali kwa nini nao hawajaweka penalty wanapochelewesha mafao ya mstaafu? (Makofi)
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, Mfuko wa NSSF unalipa 15% na hiyo ilikuwa ni riba kwa maana ya ucheleweshaji. Hata upande wa Serikali Mfuko wa PSSSF ukichelewesha mafao unalipa asilimia tano ya ucheleweshaji. Kwa hiyo, ni sahihi kwamba upande wa Serikali na Private Sectors kote kuna adhabu ikitokea kuna ucheleweshwaji, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved