Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 6 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 92 | 2025-02-04 |
Name
Antipas Zeno Mngungusi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Malinyi
Primary Question
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: -
Je, lini Serikali itatoa fedha za kukamilisha miradi ya Hospitali ya Wilaya ya Malinyi na Kituo cha Afya cha Ngoheranga?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Malinyi ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 3.6 zimetolewa na kuwezesha ujenzi wa majengo 15, ambayo yamekamilika na yanatoa huduma mbalimbali ngazi ya hospitali.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020 Serikali ilitoa shilingi milioni 570 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ngoheranga ambapo jumla ya majengo matano, ujenzi umekamilika na kituo kimeanza kutoa huduma.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu iliyosalia katika Hospitali ya Wilaya pamoja na Kituo cha Afya cha Ngoheranga, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved