Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Aleksia Asia Kamguna
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za kukamilisha miradi ya Hospitali ya Wilaya ya Malinyi na Kituo cha Afya cha Ngoheranga?
Supplementary Question 1
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA: Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Malinyi ni hospitali kubwa kweli, imejengwa vizuri na majengo mazuri sana, lakini Hospitali ile ina upungufu wa wahudumu, hasa wataalamu wa magonjwa ya wanawake (Gynaecologists). Je, ni lini Serikali itapeleka wataalamu hao?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, Kituo cha Afya cha Ngoheranga ni kituo ambacho kilijengwa kwa nguvu za wananchi walijitolea, lakini mpaka leo hakina wodi za watoto na watu wazima. Je, ni lini Serikali itaenda kusaidia kumalizia ujenzi huo? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo amekuwa akifuatilia ustawi wa wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Watanzania kwa ujumla.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu nimhakikishie kwamba, tunatambua kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita imewezesha kujenga Hospitali nzuri ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi. Tunafahamu kwamba, kila mwaka watumishi wameendelea kupelekwa ili kupunguza pengo la watumishi katika hospitali hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kibali cha mwaka huu, Mheshimiwa Rais ametoa watumishi zaidi ya 10,183 na Halmashauri ya Malinyi pia imepata watumishi hao. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie kwamba, Serikali itaendelea kuajiri kila vibali vinavyojitokeza na kuwapeleka watumishi kwenye Hospitali ya Wilaya ya Malinyi.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kuhusiana na Kituo cha Afya cha Ngoheranga, tunafahamu wananchi walitoa nguvu zao. Nitumie nafasi hii kuwapongeza wananchi wa Ngoheranga kwa kutoa nguvu zao kuchangia ujenzi wa kituo cha afya. Pia, Serikali ilipeleka shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimekamilika na kinaendelea kutoa huduma.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu ujenzi wa hivi vituo vya afya unakwenda kwa awamu; tumeanza na majengo haya matano, lakini tutaendelea na wodi nyingine ikiwemo wodi ya watoto mpaka kituo kiweze kutoa huduma zote ambazo zinahitajika ngazi ya kituo cha afya, ahsante.
Name
Tumaini Bryceson Magessa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Primary Question
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za kukamilisha miradi ya Hospitali ya Wilaya ya Malinyi na Kituo cha Afya cha Ngoheranga?
Supplementary Question 2
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Ni lini Serikali itapeleka fedha ili kukamilisha Kituo cha Afya cha Nyakagwe, Kata ya Butobela?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya ambacho kipo katika Jimbo la Mheshimiwa Magessa ni kweli Serikali ilishapeleka fedha na ujenzi umefanyika, lakini tunafahamu bado baadhi ya majengo hayajakamilika. Naomba nitumie nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaendelea na ujenzi wa hicho kituo cha afya kwa awamu na Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kupeleka na kukamilisha majengo ambayo yamesalia.
Name
Francis Isack Mtinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za kukamilisha miradi ya Hospitali ya Wilaya ya Malinyi na Kituo cha Afya cha Ngoheranga?
Supplementary Question 3
MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kituo cha Afya Ilunda kimebakiza takribani shilingi milioni 100 tu kianze kazi na mpaka sasa hakijaanza. Ni lini Serikali itatupatia fedha hizo ili kumalizia Kituo cha Afya Ilunda na wananchi waendelee kupata huduma ya upasuaji?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Kituo cha Afya cha Ilunda kilipelekewa fedha na Serikali Kuu na ujenzi wake uko zaidi ya 95%. Tunafahamu kwamba, kuna kiasi cha fedha ambacho kinahitajika kwa ajili ya ukamilishaji wa majengo hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Isack kwamba, fedha hizo zitapelekwa kupitia mapato ya Serikali. Inawezekana ikawa ni mapato ya ndani ya halmashauri au mapato kutoka Serikali Kuu, ilimradi Kituo kikamilike na kianze kutoa huduma kwa wananchi.
Name
Joseph Kasheku Musukuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Geita
Primary Question
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za kukamilisha miradi ya Hospitali ya Wilaya ya Malinyi na Kituo cha Afya cha Ngoheranga?
Supplementary Question 4
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nataka kumwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri, ni lini Serikali itapeleka shilingi milioni 125 kwa ajili ya kumalizia Kituo cha Afya Bugalama?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya Bugalama katika Jimbo la Geita Vijijini kilipelekewa fedha na Serikali na ujenzi wa majengo yake umefikia zaidi ya 90%. Tunafahamu kwamba, kuna baadhi ya majengo ambayo yanahitaji fedha hiyo shilingi milioni 123 na zaidi kidogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Musukuma kwamba, Serikali itaendelea kutafuta fedha na kupeleka kwa ajili ya ukamilishaji wa majengo hayo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved