Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 93 2025-02-04

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. REGINA N. QWARAY aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka vifaa tiba na watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ilipokea shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu, ambapo imepelekewa shilingi milioni 800. Vituo vya afya vimepelekewa shilingi milioni 600 na zahanati zimepelekewa jumla ya shilingi milioni 200.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuajiri watumishi wa kada za afya na kuwapeleka katika vituo vya huduma kote nchini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi 2024/2025, jumla ya watumishi 177 wa afya wameajiriwa na kati yao watumishi 70 wamepangwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu na wengine katika vituo vya afya na zahanati.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali ni kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, vituo vya afya na zahanati kote nchini, pamoja na kuajiri wataalamu wa kada mbalimbali za afya na kuwapanga katika maeneo yenye upungufu, ahsante.