Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. REGINA N. QWARAY aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka vifaa tiba na watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu?

Supplementary Question 1

MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa huduma ya upasuaji ni muhimu sana, hasa kwa akina mama wanapokwenda kujifungua. Wilaya ya Mbulu kwenye hii hospitali bado huduma hiyo haijaanza kwa sababu ya ukosefu wa taa za upasuaji na vitanda vya upasuaji. Je, ni lini sasa Serikali itapeleka vifaa hivyo ili huduma hii ya upasuaji iweze kuanza?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni lini Serikali itapeleka shilingi milioni 220 ili jengo la maternity ward, jengo la watoto, jengo la wanaume na jengo la wanawake yakamilike?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ni moja ya hospitali ambazo zimeanza kujengwa katika kipindi cha mwaka 2018/2019. Nilifanya ziara katika hospitali ile na niliona kwa kiasi kikubwa majengo yalikuwa hayajakamilika. Hata hivyo, kuna hatua ambazo zilichukuliwa na tukakamilisha majengo yaliyo mengi, ila bado ukamilishaji wa jengo la upasuaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri kwamba, kwa kupitia mapato ya ndani na fedha za vifaa tiba ambazo Mheshimiwa Rais amezipeleka kwenye halmashauri zote 184 katika mwaka 2024/2025 wa fedha, ambapo kila halmashauri imepata kati ya shilingi milioni 800 hadi shilingi bilioni tatu, waweke kipaumbele kwenye kununua taa kwa ajili ya jengo la upasuaji, ili jengo hilo lianze kufanya kazi kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Wilaya ya Mbulu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuhusiana na fedha shilingi milioni 200 ambazo zinahitajika kwa ajili ya ukamilishaji wodi, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itapeleka fedha hizo ili kukamilisha majengo hayo kwa ajili ya kuboresha huduma za wananchi.

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. REGINA N. QWARAY aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka vifaa tiba na watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu?

Supplementary Question 2

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunaishukuru Serikali kwa kutujengea hospitali ya Wilaya katika Kata ya Mabogini, na hospitali hii karibu inakamilika. Je, ni lini Serikali itapeleka vifaatiba na wataalamu ili wananchi wa eneo hili waanze kupata huduma?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Serikali ilipeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya mpya katika Halmashauri ya Moshi Vijijini katika Kata ya Mabogini, na niwapongeze wananchi kwa kushiriki katika ujenzi wa hospitali hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, kwamba Serikali dhamira yake ni kuhakikisha hospitali hiyo inakamilika kwa wakati, na inapelekewa vifaa tiba ili ianze kutoa huduma mapema iwezekanavyo. Kwa bahati njema, Mheshimiwa Rais ameshatoa fedha kwenye kila halmashauri katika mwaka huu wa fedha ikiwemo Halmashauri ya Moshi Vijijini.

Mheshimiwa Niabu Spika, kwa hiyo, nitumie nafasi hii kumsisitiza Mkurugenzi kuweka kipaumbele kwenye vifaatiba vya muhimu ili hospitali ianze kutoa huduma na kuhudumia wananchi ipasavyo.

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. REGINA N. QWARAY aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka vifaa tiba na watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu?

Supplementary Question 3


MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali imejenga hospitali nzuri na ya kisasa Wilaya ya Tanganyika na wakati huo huo hakuna watumishi kwenye hospitali ya wilaya na vituo vya afya, ni lini Serikali itapeleka watumishi kwenye hospitali ya wilaya sambamba na vituo vya afya?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeweka mpango mkakati wa kuajiri watumishi wa Sekta ya Afya, na pia huwapeleka katika vituo vyenye upungufu mkubwa zaidi wa watumishi. Katika Portal yetu ya ajira, watumishi wanaelekezwa zaidi maeneo ya pembezoni ikiwemo Halmashauri ya Tanganyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Kakoso kwamba Serikali katika miaka yote kuanzia mwaka 2021 mpaka sasa imeendelea kupeleka watumishi kwenye hospitali ya Wilaya ya Tanganyika pamoja na vituo vya afya na zahanati na tutaendelea kuelekeza watumishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kibali cha mwaka huu ambacho watumishi 10,183 wameajiriwa hivi karibuni, wapo ambao wameelekezwa Tanganyika, na zoezi hili ni endelevu, ahsante.

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. REGINA N. QWARAY aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka vifaa tiba na watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu?

Supplementary Question 4

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwanza, tunaishukuru Serikali kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karatu, na pia tuna vituo viwili vya afya ambavyo vina upungufu. Kituo cha Afya Kambi ya Simba na Kituo cha Afya Mbuga Nyekundu, vina upungufu wa watumishi, vifaatiba na ukosefu wa standby generator ili huduma ziweze kutolewa saa 24. Nini mkakati wa Serikali kuondoa upungufu huo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali imejenga Hospitali Halmashauri ya Karatu, Kituo cha Afya Mbuga Nyekundu na bahati njema nilifanya ziara pale, niliona ujenzi mzuri. Nimhakikishie tu kwamba safari ni hatua, tumepeleka vifaatiba kwa kiasi na mwaka huu wa fedha Mheshimiwa Rais amepeleka zaidi ya shilingi bilioni moja katika Halmashauri ya Karatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, watumishi walioajiriwa ni zaidi ya 10,183. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Paresso kwamba ni kipaumbele cha Serikali kupeleka fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba katika Hospitali ya Karatu na vituo na zahanati. Pia, tutahakikisha tunaipa kipaumbele halmashauri hiyo katika watumishi kwa kila kibali kinapotoka.

Name

Salma Rashid Kikwete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mchinga

Primary Question

MHE. REGINA N. QWARAY aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka vifaa tiba na watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu?

Supplementary Question 5

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itatupatia fedha kwa ajili ya kuboresha Zahanati ya Narumbegu kwa sababu wananchi, hasa wanawake na watoto hutoka pale na kwenda wilaya nyingine kwa ajili ya kupata huduma ya afya? Ahsante sana.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie nafasi hii kumpongeza mama yangu Mheshimiwa Salma Kikwete, kwanza kwa kazi nzuri ambayo ameifanya na nafahamu Serikali ya Awamu ya Sita hivi karibuni imepeleka zaidi ya shilingi milioni 600 katika Kituo chake cha Rutamba ambacho amekuwa anakisemea muda mrefu.

Mheshimiwa naibu Spika, pia nimhakikishie tu kwamba katika Zahanati hiyo ya Narumbegu na maeneo mengine yote ya kimkakati ambayo ni vijiji vyenye idadi kubwa ya wananchi na umbali mkubwa kwenda kwenye vituo vingine vya huduma, tutahakikisha tunaweka kipaumbele kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati na vituo vya afya. Kwa hiyo, eneo hilo tumelichukua na tutalifanyia kazi.