Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 95 2025-02-04

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMAR M. KIGUA aliuliza:-

Je, upi mpango mkakati wa kufikisha nishati ya umeme kwenye maeneo yote ya uchimbaji wa Madini – Kilindi?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Kilindi ina maeneo yapatayo 12 ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ambapo kati ya hayo, maeneo manne tayari yameshapatiwa huduma ya umeme. Maeneo hayo ni Mafulila, Mfyalime/Najim, Masagulu Muheza na Chanungu.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, eneo la Matanda, mkandarasi aitwaye DIEYNEM Company Ltd anaendelea na kazi ya kuweka miundombinu ya umeme na anatarajia kukamilisha kazi hiyo hivi karibuni. Maeneo mengine yaliyosalia yatapata umeme kupitia miradi mbalimbali itakayofuata, ahsante.