Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMAR M. KIGUA aliuliza:- Je, upi mpango mkakati wa kufikisha nishati ya umeme kwenye maeneo yote ya uchimbaji wa Madini – Kilindi?

Supplementary Question 1

MHE. OMAR M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuishukuru Serikali kwa kuweza kupeleka umeme kwenye maeneo manne ambayo yalikuwa yana uhitaji mkubwa sana kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Je, ni lini sasa maeneo nane yaliyobaki yataweza kupelekewa umeme?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kwamba, tuna Mradi wa Gridi Imara ambao unaanzia Mkata hadi Kilindi kwa ajili ya kuimarisha umeme maeneo mbalimbali, lakini mradi huo umesimama. Je, nini mpango mkakati wa kuhakikisha kwamba mradi ule unaendelea? Ahsante.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na maeneo nane ambayo yamebakia, Serikali inayo miradi ambayo tutaianza mwaka huu wa fedha. Kwa maeneo haya nane ya Mheshimiwa Mbunge, nitakaa na REA na kuwaambia katika maeneo ambayo tunayatenga kupeleka umeme kwenye vitongoji, basi na maeneo ambayo vitongoji hivi vinapita waweze kupata umeme kwa ajili ya kuimarisha shughuli hizo za uchimbaji katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Mradi wa Gridi Imara wa Mkata na Kilindi tutahakikisha tunaendelea na mazungumzo na wenzetu wa Wizara ya Fedha ili fedha ziweze kutoka kwa ajili ya kuendelea kutekeleza miradi hiyo, ahsante.

Name

Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Primary Question

MHE. OMAR M. KIGUA aliuliza:- Je, upi mpango mkakati wa kufikisha nishati ya umeme kwenye maeneo yote ya uchimbaji wa Madini – Kilindi?

Supplementary Question 2

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, Kiteto umeme ulikuwa unakatika sana, mara kwa mara, na ni kwa muda mrefu sasa, na imeleta madhara ya kuunguza vifaa vya wananchi. Nini kauli ya Serikali? Nashukuru.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunao utaratibu wa kuwalinda walaji kupitia EWURA, ambapo mwananchi ambaye amepata athari kutokana na matumizi ya umeme, kuna utaratibu wa kufuata kuleta malalamiko, na kisha kuna utaratibu wa kuyafanyia kazi na kuona kama anastahili kupewa fidia au vinginevyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namshauri Mheshimiwa Mbunge na wananchi kutoka kwenye jimbo lake tufuate utaratibu ambao tunao, mwananchi yeyote ambaye amepata athari hii, upo utaratibu wa kupata haki yake, ahsante.