Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 96 2025-02-04

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: -

Je, lini Serikali itamaliza kusambaza umeme kwenye vitongoji nchini?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia tarehe 15 Januari, 2025, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imekamilisha kupeleka umeme kwenye vijiji vyote 12,318 nchini. Aidha, Serikali imepeleka umeme kwenye vitongoji 33,657 kati ya vitongoji 64,359 sawa na 52.3%. Vitongoji 30,702 vilivyobaki vipo kwenye mpango wa kupatiwa umeme kupitia miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji ambapo Serikali imeandaa Mpango wa kupeleka umeme katika vitongoji 20,000 kwa kipindi cha kati ya miaka mitano mitano hadi kumi 10 kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024. Mpaka sasa vitongoji 4,020 vipo katika Mpango wa utekelezaji kupitia miradi mbalimbali. Serikali inajipanga katika miradi mingine ya kupeleka umeme vitongojini kulingana na miradi itakayofuata, ahsante.