Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 98 2025-02-04

Name

Nashon William Bidyanguze

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza: -

Je, miradi mingapi ya umwagiliaji imepangwa kujengwa Wilayani Uvinza kwa mwaka wa fedha 2023/2024?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Wilaya ya Uvinza ilikuwa na miradi minne ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika Skimu za Kashagulu, Mgambazi, Nkonkwa na Ilagala. Aidha, hatua za manunuzi kwa ajili ya kumpata mshauri elekezi wa kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu zimekamilika na kazi za upembuzi yakinifu zitaanza mara baada ya hatua za kimkataba kukamilika, ahsante sana. (Makofi)