Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nashon William Bidyanguze
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Kusini
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza: - Je, miradi mingapi ya umwagiliaji imepangwa kujengwa Wilayani Uvinza kwa mwaka wa fedha 2023/2024?
Supplementary Question 1
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, miradi anayoitaja ya Kashagulu yote ilikuwepo. Sasa, nataka atoe ufafanuzi ili wananchi wangu wasikie na waelewe kwa nini inatajwa kama ndiyo miradi ambayo nimeiuliza?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kuna miradi ambayo ilianzishwa katika Kijiji cha Nyanganga, Itebula pamoja na Nguruka mpaka sasa bado haijakamilika na ni muda mrefu sana. Je, ni lini miradi hii nayo itakwenda kukamilishwa? Ahsante. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza namthibitishia Mheshimiwa Mbunge wa Uvinza kwamba mradi kama wa Kashagulu ambao ulijengwa zamani haukuwa umefuata zile taratibu za ujenzi na hauja-cover eneo kubwa kama inavyotakiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais alituelekeza sisi kuhakikisha tunapitia miradi yote ya zamani na kujenga miradi mipya, ndiyo maana katika jimbo lake, moja ya miradi ambayo tunapitia ni pamoja na Mradi wa Kashagulu. Tunataka kuujenga kisasa na tunaupanua ili uweze kuhudumia wananchi wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu miradi ya maeneo ya Nguruka na Itebula na yenyewe tutaiingiza katika mpango unaofuatia kwa sababu tunafanya kwa awamu kulingana na bajeti ambayo Serikali inakuwa imetupangia. Kwa hiyo, na lenyewe uwathibitishie wananchi wa Uvinza kwamba hili litafanyika chini ya Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Name
Dr. Pius Stephen Chaya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Mashariki
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza: - Je, miradi mingapi ya umwagiliaji imepangwa kujengwa Wilayani Uvinza kwa mwaka wa fedha 2023/2024?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, mwaka 2024 Serikali ilifanilkiwa kutangaza tenda mbili za ujenzi wa Miradi ya Umwagiliaji wa Mbwasa na Udimaa. Taarifa niliyonayo ni kuwa wakandarasi walishapatikana. Je, ni lini wakandarasi wataenda site kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hizo schemes?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo la Manyoni ambako anatokea Mheshimiwa Dkt. Chaya, tayari miradi hiyo wakandarasi wamepatikana na nimwambie tu kwamba mwezi uliopita Januari, mwishoni Serikali ilishatoa fedha (advance payment) kwa ajili ya kuanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, Mradi wa Mbwasa anajenga mkandarasi anaitwa Tonde Construction ambaye tayari ameshapatiwa karibu shilingi bilioni moja za awali na anafanya organisation kwa ajili ya kuingia site. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza: - Je, miradi mingapi ya umwagiliaji imepangwa kujengwa Wilayani Uvinza kwa mwaka wa fedha 2023/2024?
Supplementary Question 3
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Kata ya Isebya, Kijiji cha Mgelele tuna mradi wa kilimo toka mwaka 2023 tunauingiza kwenye bajeti. Serikali itatoa lini fedha ili utekelezaji wa mradi huo wa kilimo uanze? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo la Mbogwe ambako anatokea Mheshimiwa Maganga, tunatambua kuhusu huo mradi, na ni kweli kwamba tunachotafuta sasa hivi ni fedha. Wizara ya Fedha imeshatuahidi kwamba itatupatia fedha katika mgao unaofuatia, maana yake tutatoa kwa ajili ya huo mradi kukamilika. Kwa hiyo, waondoe shaka wananchi wako jambo hilo litafanyika, ahsante. (Makofi)
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza: - Je, miradi mingapi ya umwagiliaji imepangwa kujengwa Wilayani Uvinza kwa mwaka wa fedha 2023/2024?
Supplementary Question 4
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi, nami niulize swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na agizo la Serikali la kufufua zao la kahawa Mkoani Kilimanjaro, ipo mikakati mbalimbali inayowezesha kufufua zao hili ikiwemo kuboresha mifereji ambayo inapeleka maji katika mashamba hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata ya Old Moshi Mashariki, tangu mwaka 2009 walilaza mabomba na Serikali ilitoa shilingi milioni 240, mabomba yale yanaharibika. Nataka kujua ni nini kauli ya Serikali ya kuendeleza mifereji hii ili wananchi waweze kumwagilia zao hili na Serikali iweze kupata kipato? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, Nimwondoe shaka Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Felista Njau, vilevile, namtambua Mbunge wa Jimbo. Ni kwamba eneo hilo la Moshi Vijijini kuna kazi nzuri ambayo Serikali imeifanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, kauli ya Serikali ni kwamba tumeshaielekeza Tume ya Umwagiliaji kupitia mkoa kwamba wafanye feasibility study ili kujua gharama halisi za mradi ili tuje kuleta yale mabomba kwa ajili ya kusaidia wakulima wa kahawa katika Mkoa wa Kilimanjaro hasa katika Kata za Old Moshi. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved