Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 99 2025-02-04

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Barabara ya Mkuzi hadi Mlola Lushoto kwa mkupuo mmoja kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Magamba – Mkuzi hadi Mlola (kilometa 35.37) unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa 5.33 kuanzia Magamba hadi Mkuzi zimejengwa kwa kiwango cha lami. Kwa sehemu iliyobaki ya kutoka Mkuzi hadi Mlola (kilometa 30.04), Serikali itaendelea kuijenga kwa kadiri ya fedha zinavyopatikana, ahsante. (Makofi)