Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Barabara ya Mkuzi hadi Mlola Lushoto kwa mkupuo mmoja kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 1
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi, na pia nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Nina maswali mawili ya nyongeza. Wakati Serikali inatafuta fedha, kwa nini isitenge fedha za dharura kutengeneza maeneo korofi ili wananchi waweze kupita hasa kipindi hiki cha mvua?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, barabara hiyo hiyo sehemu ya Kwai ina sharp corner (kona kali) na husababisha magari ya mizigo kushindwa kuzunguka pale. Je, Serikali haioni kwamba kuna haja ya kujenga daraja maeneo yale ili kukwepa kupita eneo hilo la kona kali? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kwa pamoja, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, natoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS wa Mkoa wa Tanga, aweze kufika kwenye barabara ya Mheshimiwa Mbunge na kuainisha maeneo yote ambayo yamekuwa korofi hasa katika kipindi hiki cha mvua ili aweze kuyakarabati, na ikiwezekana aweze kuleta taarifa Wizarani ili wananchi waweze kuhakikisha kwamba wanapita katika eneo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu eneo la Kwai ambalo Mheshimiwa Mbunge anasema kuna kona kali, kwa kuwa Meneja atakwenda maeneo hayo aweze kufanya tathmini kama kuna uhitaji wa kujenga hilo daraja, basi aweze kuleta taarifa Wizarani ili mipango iwekwe kwa ajili ya kujenga hilo daraja eneo hilo lenye kona kali. (Makofi)
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Barabara ya Mkuzi hadi Mlola Lushoto kwa mkupuo mmoja kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 2
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo ni mara ya tisa nauliza swali hili kwa Mheshimiwa Naibu Waziri. Ni lini mshauri ambaye alitangaza hapa Bungeni kwamba ataniambia anaenda kuanza kazi ya upembuzi yakinifu wa barabara ya kutoka Kahama – Nyang’hwale – Busisi ili ijengwe kwa kiwango cha lami? Lini atatutangazia kuwa mpembuzi anaanza kazi? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba baada ya hapa niweze kupata taarifa, lakini nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari hatua za manunuzi zilishaanza. Kuhusu ni lini ataanza, labda baada ya hapa niweze kutoka nijiridhishe ili nimpe tarehe na mwezi ambao hakika atakuwa yuko uwandani kwa ajili ya kufanya kazi ya upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa kina. (Makofi)
Name
Josephine Johnson Genzabuke
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Barabara ya Mkuzi hadi Mlola Lushoto kwa mkupuo mmoja kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iliahidi kuwalipa fidia wananchi wa Mnanila ambao vibanda vyao vilibomolewa. Je, ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi hao wa Mnanila Wilaya ya Buhigwe ambao ahadi yao ilitolewa mbele ya Makamu wa Rais?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba wananchi hao wamefika mara kadhaa katika Wizara kufuatilia hiyo fidia na mpaka sasa hivi tunaendelea na majadiliano nao hasa wale ambao walikutwa nje ya eneo lenyewe. Kwa hiyo, Serikali tumeendelea kufanya mazungumzo pamoja na wenzetu wa mkoa ili kuona kama hawa wananchi walikuwa na haki au wao ndio walikuwa wameingia kwenye Barabara, ahsante. (Makofi)
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Barabara ya Mkuzi hadi Mlola Lushoto kwa mkupuo mmoja kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 4
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Barabara ya kutoka Iringa – Dodoma imechoka sana, ina mashimo mengi, haina hadhi ya barabara ya kuunganisha mkoa na mkoa. Ni lini Serikali itajenga upya barabara hii? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge, siyo barabara hiyo tu, ziko barabara nyingi ambazo kwa kweli zinahitaji matengenezo makubwa ikiwepo hiyo Barabara ya Iringa – Dodoma.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari sasa hivi tuko kwenye mipango ya kuhakikisha kwamba barabara zote ambazo muda wake umepita ama zimechoka, tuweze kuziingiza kwenye mpango hasa hizi barabara kubwa za kiuchumi ili tuweze kuzitengeneza zirudi katika ubora wake unaostahili. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved