Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Works and Transport Wizara ya Uchukuzi 100 2025-02-04

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. CONDESTER M. SICHALWE aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani kwa kushirikiana na Serikali ya DRC kuanzisha usafiri wa kufika Lubumbashi kupita Ziwa Tanganyika?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA UCHUKUZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) inakamilisha miradi ya ukarabati wa meli zake tatu ambazo ni MV Liemba na MV. Mwongozo zitakazofanya kazi kati ya Bandari za Kigoma na Karema kwa upande wa Tanzania na Bandari ya Kalemie kwa upande wa DRC na siyo Lubumbashi. Aidha, Serikali ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wa meli mpya ya abiria na mizigo itakayofanya kazi kati ya nchi hizo mbili, ahsante.