Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. CONDESTER M. SICHALWE aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kwa kushirikiana na Serikali ya DRC kuanzisha usafiri wa kufika Lubumbashi kupita Ziwa Tanganyika?

Supplementary Question 1

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Lubumbashi ambayo jimbo lake kuu ni Haut-Katanga ni kati ya majimbo tajiri sana kwenye Nchi ya DRC na ni miongoni mwa jimbo ambalo Watanzania wengi wanalitumia kwa sababu hakuna vita…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa twende kwenye swali la nyongeza.

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ikiwa wamekamilisha meli hizo kupitia Ziwa Tanganyika, mpango wa barabara baada ya kumaliza Ziwa Tanganyika kuelekea Lubumbashi umefikia wapi? Ndiyo hoja kubwa iko hapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ikiwa Bandari ya Karema imejengwa kwa zaidi ya shilingi milioni 49 na imekamilika na mpango wa kujenga Bandari ya Karema ulikuwa ni kuepusha mlolongo wa kutoka Bandari ya Kalemie upande wa DRC ili kupatikane Bandari ya Moba; mpaka sasa hivi DRC hawana Bandari ya Moba, sisi tija ya kujenga bandari hii upande wa kwetu yenye zaidi ya shilingi trilioni 49 ni nini?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tuna mahusiano mazuri na wenzetu wa DRC na tunafanya shughuli nyingi kwa pamoja. Tunapoongea sasa hivi ni kwamba bahati nzuri wenzetu wa DRC na sisi hasa Wizara ya Ujenzi tuna timu ya pamoja ambayo inapitia uwezekano wa kujenga barabara kutoka kwenye bandari za upande wa DRC kwenda Lubumbashi. Tayari tuna timu ambayo inafanya hizo kazi, kwa hiyo, iko kwenye taratibu hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, itaangaliwa kama kutakuwa na tija na hiyo Barabara, basi tutasaidiana nao au tutatafuta utaratibu wa namna ya kuijenga hiyo barabara na wenzetu wa DRC…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hokororo.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Kuhusu Bandari ya …

NAIBU SPIKA: Endelea Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Bandari ya Karema, haijafanya kazi vizuri sana, lakini tunavyoongea sasa hivi kwa upande wetu, Serikali tuna wakandarasi wawili ambao tumewa-engage kujenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mpanda – Karema na tayari wako site. Kwa hiyo, meli hizo zitakapokuwa zimekamilika, zinaweza kwenda kwenye bandari yoyote upande wa pili pale ambapo tutakuwa tumekamilisha barabara upande wetu na kwao kule. Kwa hiyo, taratibu zipo zinaendelea vizuri kati yetu na wenzetu wa DRC, ahsante.

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CONDESTER M. SICHALWE aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kwa kushirikiana na Serikali ya DRC kuanzisha usafiri wa kufika Lubumbashi kupita Ziwa Tanganyika?

Supplementary Question 2


MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina utaratibu gani wa kurejesha usafiri wa meli baada ya Bandari ya Mtwara na Dar es Salaam kuimarika? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunakiri kwamba tulikuwa na usafiri huo, lakini baada ya kuwa na usafiri mzuri wa Barabara, tutaangalia uwezekano kama tukiwa na usafiri wa abiria wa meli itakuwa na tija ili tuweze kurejesha usafiri huo.